Wednesday, September 14

Chuo cha Mipango (IRDP) kufungua tawi katika jiji la Mwanza



Chuo cha Mipango cha Mjini Dodoma kinatarajia kufungua tawi jipya katika Mkoa wa Mwanza hivi karibuni, ili kuongeza udahili wa wanachuo wanaochukua Astashahada ya Mipango Vijijini.
Hatua hiyo inalenga kuzalisha wataalamu wengi watakaosaidia kuzalisha wataalamu wengi wa sekta ya mipango wataowezesha wananchi kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi ya kijjiji hadi taifa.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Ofisa Masoko na Mahusiano wa Chuo cha Mipango cha Dodoma, Godrick Ngoli, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kwenye banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya wakulima ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika mkoani hapa.
Alisema kimsingi masomo katika tawi la Mwanza yangeanza Julai, lakini kutokana na utaratibu wa uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia wamelazimika kusogeza mbele hadi Septemba mwaka huu ambapo ndio mwaka wa masoko kwa tawi hilo utakapoanza.